Alhamisi, Agosti 21, 2014

JIANDAE NA NGOMA MPYA YA BEN POL JUMATATU

Ben Pol amepanga kuachia wimbo mpya Jumatatu ya wiki ijayo ambao ameufanya katika studio za Noiz Mekah, chini ya producer DX.
Ben Pol ameeleza kuwa wimbo huo utatoka maalum kwenye mtandao wa Mkito hivyo utakuwa ukinunuliwa online.
Kwa mujibu wa Ben Pol, yeye na DX walikubalina kuwa wimbo huo utakuwa wa kwao wote katika biashara hiyo kwa maana kwamba watagawana.

0 comments:

Chapisha Maoni