Mwanawe muigazaji nyota wa Hollywood Jackie Chan amekamatwa kwa madai alitumia mihadarati.
Jaycee Chan, 31, ambaye mwenyewe ni msanii
pamoja na muigizaji kutoka Taiwanese Kai Ko, 23, walikamatwa alhamisi
iliyopita kwa mujibu wa taarifa ya polisi mjini Beijing .
Polisi
wanasema kuwa wawili hao walipatikana wamevuta bhangi huku mwanawe Chan
akikabiliwa na kosa zaidi la kupatikana na dawa hiyo haramu.
Kukamatwa kwa wawili hao kunawadia wakati polisi wamekuwa wakifanya misako ya dharura na kuwakamata wasanii nyota kadhaa.
Gao Hu, 40, aliyeigiza katika filamu ya mwaka
wa 2011 Zhang Yimou "The Flowers of War", alikuwa miongoni mwa wasanii
wengine wakutajika waliokamatwa mapema mwezi huu.
HU alipatikana ametumia Bhangi pamoja na madawa aina ya methamphetamines.
Operesheni hizi zinafuatia agizo la rais wa
China Xi Jinping mwezi juni kwa polisi la kuwataka kuimarisha juhudi
za kukabiliana na matumizi ya mihadarati nchini humo.
Duru zinaarifu kuwa Kukamatwa kwa mwanawe msanii
maarufu zaidi nchini humo maafisa wa polisi wanajaribu kuwadhibitishia
umma kuwa hakuna atakayeepuka mtego wao .
Mwandishi wa BBC mjini Beijing Martin Patience
anasema kuwa watu wenye sifa kubwa wanalengwa na maafisa wa polisi
kutokana na ushawishi mkubwa walionao miongoni mwa jamii nchini humo.
Hata
hivyo kiongozi wa idara ya baraza la umma la Beijing inayopambana na
matumizi ya mihadarati bwana Jin Zhihai amekanusha kuwa idara yake
imekuwa ikilenga wasanii na waigizaji nyota katika kampeini yao dhidi
ya matumizi ya mihadarati.
ikiwa tutaendelea na kampeini hii dhidi ya matumizi ya mihadarati ninahakika waigizaji wengi nyota watakamatwa
Juma lililopita miungano 42 inayowakilisha
wasanii walitia sahihi maagano ya kukataa kuwasajili wasanii waotumia
mihadarati katika maonesho yao.
Kampuni inayomwakilisha bwana Chan iliomba msamaha kwa uma kwa niaba yake.
Kampuni hiyo ya M'Stones International iliahidi kumpeleka hospitalini ilikukomesha matumizi ya dawa hizo.
Babake Jackie Chan hajasema lolote kufikia sasa.
0 comments:
Chapisha Maoni