Jumanne, Agosti 12, 2014

DRC YAPAMBANA NA WAASI

Mapigano makali yameshuhudiwa kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na wanamgambo wa Mai-Mai katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo. Taarifa zinasema kuwa, mapigano hayo yalitokea katika eneo moja kaskazini mwa mkoa wa Kivu Kaskazini. Duru za jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimetangaza kuwa, mapigano hayo yalijiri kati ya jeshi la nchi hiyo na wanamgambo wa Mai-Mai Cheka. Taarifa zaidi zinasema kuwa, jeshi la Congo limefanikiwa kuwafurusha wanamgambo hao kutoka katika maeneo hayo. Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limefanikiwa katika mapigano hayo kuangamiza silaha za wanamgambo hao na kwamba, sasa jeshi hilo linayadhibiti maeneo hayo.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, hivi karibuni Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilieleza wasiwasi wake juu ya kuongezeka machafuko katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamekuwa yakikabiliwa na machafuko ya mara kwa mara kutokana na kuweko harakati za makundi ya waasi.

0 comments:

Chapisha Maoni