Waislamu wa India ambao wamekimbia nyumba na makazi yao katika jimbo la
Uttar Pradesh huko kaskazini mwa nchi hiyo wameripotiwa kuwa katika hali
mbaya na ya kusikitisha.
Ripoti zinasema kuwa idadi kubwa ya Waislamu wa jimbo la Uttar Pradesh wanasumbuliwa na hali mbaya katika kambi za wakimbizi na hawako tayari kuondoka kwenye kambi hizo kutokana na woga wa kuuliwa. Waislamu hao wanawatuhumu viongozi wa jimbo hilo kuwa wanawaunga mkono mahasimu wao kwa sababu za kisiasa.
Wahindu wenye misimamo mikali walianzisha mashambulizi na ghasia dhidi ya Waislamu wa jimbo la Uttar Pradesh Disemba mwaka jana na hadi sasa makumi ya Waislamu wameuawa na wengine zaidi ya elfu 50 kuwa wakimbizi.

0 comments:
Chapisha Maoni