Jumatano, Julai 23, 2014

HAJI ADAM AUKANDIA UONGOZI WA BONGO MOVIE!

Nyota wa filamu za Kibongo, Haji Adam ‘Baba Haji’ amewatupia dongo kiaina viongozi waliopita kwenye Klabu ya Bongo Movie Unity kwa kuusifia uongozi wa sasa wa klabu hiyo unaoongozwa na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.Akipiga stori mbili tatu na mwandishi wetu, Baba Haji alisema kuwa uongozi wa Steve umeleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya filamu Bongo kwa kuwa wamekuwa na umoja na ushirikiano katika masuala ya kijamii tofauti na uongozi uliopita.
Nafurahi kuwa na kiongozi mwenye kujali maendeleo na kuwa na msimamo ambao umetufikisha mbali na kutufanya tuwe na ushirikiano kwenye matatizo mbalimbali yanayotupata wana Bongo Movie
alisema Baba Haji.
Uongozi uliopita wa Bongo Movie Unity ulikuwa chini ya Vincent Kigosi ‘Ray’ ambaye alipokea kijiti hicho kutoka kwa Jacob Steven ‘JB’.

0 comments:

Chapisha Maoni