Watafiti katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Temple,
Marekani wamegundua dawa ya kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambayo ni
ya uhakika zaidi ukilinganisha na zilizowahi kupatikana katika tafiti
za awali duniani.
Dawa yao inaweza kutumika kwa tiba ya wanaoishi na VVU na kinga kwa wale ambao bado hawajaambukizwa.
Mmoja wa watafiti hao, Dk Kamel Khalili aliwaambia
waandishi wa habari juzi mjini Philadelphia, Marekani kuwa tofauti na
utafiti mwingine, wao wamegundua namna ya kukiondoa kirusi kilichoingia
kwenye kinasaba (DNA) ndani ya CD4 na kukitoa nje na hatimaye kukiua.
Alisema dawa hiyo inafanya kazi hiyo bila kuathiri seli za mwili wa binadamu.
Dk Khalili alisema ugunduzi wao ni wa hali ya juu
zaidi kwa sababu teknolojia ya kutengeneza dawa hiyo ni tofauti na
nyingine zilizokwisha kugunduliwa ambazo hazina uwezo wa kupenya ndani
ya seli za binadamu, bali kuathiri tu VVU vilivyopo nje yake, ndani ya
mfumo wa damu.
0 comments:
Chapisha Maoni