MKURUGENZI wa RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’
ameshindwa kumzika baba mdogo wa mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo,
Blandina Chagula, Clement Kiyenze Chagula.Mzee huyo alifariki katika
Hospitali ya Muhimbili kutokana na matatizo ya presha na figo yaliyokuwa
yakimsumbua na kuzikwa katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo
wasanii mbalimbali wa filamu nchini walishiriki akiwemo Mbunge wa
Chalinze, Ridhiwani Kikwete.Alipoulizwa Ray kwa nini hakuhudhuria mazishi hayo, alisema:
Ukweli ni kwamba mimi sipo Dar. Ndiyo maana sijaonekana huko kwenye mazishi, nipo Mwanza katika shughuli zangu za kikazi, tuko pamoja lakini
alisema Ray.
0 comments:
Chapisha Maoni