Mcheza filamu kutoka Bongo Movies, Yobnesh Yusuph
‘Batuli’ amefunguka kuwa anaumia kuona listi ndefu ya Wabongo
wanaosubiri kunyongwa nchi mbalimbali kwa kukutwa na dawa za kulevya.
Batuli
alisema kinachowaponza vijana wengi ni kupenda fedha za chapuchapu,
matokeo yake wanaambulia kifungo cha maisha na wengine kunyongwa katika
nchi zenye misimamo mikali.
Inashangaza sana wasichana wanaingia katika biashara hii haramu, mbaya zaidi wanapoingiza madawa ya kulevya wanaharibu kizazi kilichopo, inaniuma sana maana vizazi na vizazi vinaendelea kuangamia
alisema
Butuli.
0 comments:
Chapisha Maoni