Wakulima wa mahindi zaidi 50 wa kata ya Ruaha Manispaa ya Iringa wamepata mafunzo ya siku mbili ya ujasiriamali wa kilimo bora ili kuinua kipato chao.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Renatusi Mushi amesema mafunzo hayo yamelenga kuwaelimisha wakazi wa kata ya Ruaha juu ya kukabiliana na changamoto ya umasikini kupitia kilimo.
Bw. Mushi amesema mafunzo hayo yatawasaidia wakazi wa kata ya Ruaha kujua njia bora kilimo na namna ya kupata soko la ndani na nje ya nchi la mazao yao ili kuinua kipato chao.
Aidha, amesema kilimo bora ndiyo njia pekee ya mwananchi kujikomboa kiuchumi kwani kitawawezesha kupata chakula cha kutosha na kuongeza pato lao.
Naye mmoja wa wakulima hao Bi Emelda Chuhila ameshukuru kupata mafunzo hayo ambapo amesema yatawasaidia kujikwamua kiuchumi na kupunguza ukali wa maisha.
Hata hivyo, Mtaalamu huyo wa masuala ya kilimo Bw. Renatusi Mushi amewataka wakulima kujitokeza kwa wingi pindi kunapokuwa na mafunzo ya ujasilimia mali ambayo mara nyingiyamekuwa yakitolewa bure lakini yana umuhimu wa kuboresha maisha ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla.

0 comments:
Chapisha Maoni