Jumatano, Julai 23, 2014

ZAHANATI 9 KUANZA KUTOA HUDUMA YA AFYA KWA JAMII IRINGA

Jumla ya Zahanati 9 Mkoani Iringa zipo katika hatua mbalimbali za ujenzi ili kuanza kutumika kutoa huduma ya afya kwa jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma amesema serikali ya Chama cha Mapinduzi imeendelea kufanya jitihada za kuboresha huduma za kijamii ikiwemo afya katika kutekeleza ilani ya chama hicho.
Dkt. Ishengoma amesema zahanati zote hupewa dawa na wataalamu hupewa elimu kila wakati ili kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Aidha amesema katika suala la elimu ya sekondari serikali imeendelea kushirikiana na wananchi ambapo wamejenga vyumba kadhaa vya madarasa ili kurahisisha upatikanaji wa elimu kwa watoto wao.
Hata hivyo, mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma amesema taarifa hiyo ni tathimini ya utekelezaji wa ilani ya chama tawala ya mwaka 2010 kutoka mwezi Januari hadi Julai mwaka huu.

0 comments:

Chapisha Maoni