Madaktari nchini India wametoa meno 232
kutoka katika mdomo wa kijana mwenye umri wa miaka 17, katika upasuaji
uliochukua saa saba.
Kijana huyo Ashik Gavai alifikishwa hospitali akiwa amevimba na maumivu kwenye taya na shavu lake la upande wa kulia, amesema Dokta Sunada Dhiware, mkuu wa idara ya meno katika hospitali ya JJ jijini Mumbai.
Kijana huyo amekuwa akisumbuliwa kwa miezi 18, na alilazimika kusafiri kwenda mjini, baada ya madaktari katika kijiji chake kushindwa kufahamu chanzo cha tatizo.Kijana huyo Ashik Gavai alifikishwa hospitali akiwa amevimba na maumivu kwenye taya na shavu lake la upande wa kulia, amesema Dokta Sunada Dhiware, mkuu wa idara ya meno katika hospitali ya JJ jijini Mumbai.
Madaktari wameelezea hali hiyo kuwa
ni haba sana kutokea na ni jambo ambalo limevunja rekodi ya dunia.
Ashik sasa ana meno 28.
Ashik aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa aina yake ambao ufizi mmoja huunda meno mengi. Ni kama aina ya uvimbe wa saratani
amesema Dokta
Dhiware.
Mwanzoni, hatukuweza kukata fizi, kwa hiyo tulilazimika kutumia nyundo na tindo kufanikisha.
Tulivyopasua tu, meno madogo madogo yakaanza kutoka, moja baada ya jingine, na tulipoyahesabu, yalifika meno 232.
Amesema daktari huyo.
0 comments:
Chapisha Maoni