Alhamisi, Julai 03, 2014

VIDEO YA KEREWA KATIKA KIOO CHA MTV BASE

Inagharimu pesa nyingi na nguvu nyingi kwa msanii kutoka Tanzania kufanya video na kampuni kubwa za Africa kama kampuni ya Godfather inayofanya kazi zake nchini Afrika Kusini. Shetta amefanikiwa kufanya kazi na Godfather kwenye video yake ya “Kerewa” aliyomshirikisha Diamond Platnumz.
Video imekwisha anza kuchezwa Tanzania na sasa kwenye kituo cha television cha Mtv Base nao wameanza kuicheza video hii.
Fahamu ili Mtv Base kucheza video yako ni lazime iwe kwenye kiwango cha kimataifa na wimbo ukithi viwango vyao, ndio maana wasanii hugaramika sana kufanikisha video zao kuchezwa kwenye vituo vinavyorusha matangazo yao Africa Nzima kama Mtv Base.

0 comments:

Chapisha Maoni