Alhamisi, Julai 03, 2014

AMBAKA MAMA YAKE MZAZI NA KUMUUA MBEYA

MTU anayedhaniwa kuwa ni mgonjwa wa akili, amembaka na kumuua kwa kumpiga fimbo kichwani na usoni kisha kumnyonga shingo mama yake mzazi mwenye miaka 73, mkazi wa Kijiji cha Ibungila wilayani Rungwe, mkoani hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alimtaja mtuhumiwa kuwa ni Kiswigo Anganisye (33), mkazi wa kijiji hicho.
Alisema kuwa, tukio hilo limetokea juzi, majira ya saa 6:30 usiku, ambako inadaiwa kuwa, kabla ya kuuawa, marehemu pia alibakwa na mtuhumiwa.
Hata hivyo, Kamanda Msangi alisema kuwa, chanzo cha tukio hilo, inadaiwa kuwa ni baada ya marehemu kumpikia mtuhumiwa magimbi badala ya ugali, ndipo alipochukia na kuchukua uamuzi huo na kwamba amekamatwa na anashikiliwa na jeshi hilo.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi mkoani hapa, linawashikilia raia wawili wa Malawi kwa kosa la kuingia nchini kinyume na utaratibu.
Watuhumiwa hao ni Thomas Juma (29), na Boniface Chitete (29), wote wakazi na raia wa Malawi.
Kwa kujibu wa Kamanda Msangi, watuhumiwa hao walikamatwa juzi majira ya saa 3:15 usiku, baada ya msako uliofanyika Kyela mkoani hapa na taratibu za kuwakabidhi Idara ya Uhamiaji zinafanyika.

0 comments:

Chapisha Maoni