Vijana wilayani Mbarali wameiomba serikali kutangaza tatizo la
matumizi ya vipodozi vyenye viambata vya sumu na pombe haramu za viroba
kuwa janga la kitaifa kama ilivyo kwa dawa za kulevya kutokana na
matumizi ya bidhaa hizo kuwa na madhara makubwa kwenye sekta ya afya na
uchumi wa taifa.
Wakizungumza wakati wa zoezi la kuteketeza vipodozi vyenye viambato
vya sumu na pombe haramu za viroba ambalo limefanywa na mamlaka ya
chakulana dawa (TFDA) wilayani Mbarali, vijana hao wamesema pombe hizo
za viroba zimesababisha vijana wengi wilayani humo kupoteza maisha, huku
vipodozi vyenye viambato vya sumu pia vikiathiri vibaya ngozi za
watumiaji, hali ambayo inawasukuma kuiomba serikali kuotangaza bidhaa
hizo kuwa janga la kitaifa.
Kaimu meneja wa mamlaka ya chakula na dawa kanda ya nyanda za juu
kusini, Yusto Walace amesema TFDA itaendelea kudhibiti bidhaa hizo
haramu huku baadhi ya maofisa wa serikali wilayani mbarali wakielezea
changamoto zinazowapata katikakukabiliana na bidhaa hizo.
Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Gulam Hussein Kifu amekiri kuwepo kwa
bidhaa hizo kwa wingi wilayani Mbarali na kuitaka TFDA kutumia vyombo
vya dola kuendeleza mapambano ya kuzidhibiti ili kupunguza madhara yake
kwa vijana.
0 comments:
Chapisha Maoni