Leo Julai 3, 2014 ni siku ya kuzaliwa ya msanii na mwanamuziki wa kitanzania, Rama Dee ambaye kwa sasa makazi yake yapo nchini Australia, haya ameyasema kupitia mtandao wake wa facebook:
Siku ya leo ni kubwa kwangu Ndugu….leo tar 03/07 ni siku yangu ya kuzaliwa, siku kama hii mwaka jana nilifanya wimbo na LedyJadee wa "Kama Huwezi" nasikia furaha sana kuona Mungu bado yupo nasi kwenye shida na raha haswa upande wa shida,kufika asubuhi na kuona mwanga wa "Jua" sio kitu rahisi, so tuna wajibu wa kushukuru….pia napenda kuwapongeza kwa wale wooote walio zaliwa siku kama ya leo mfahamu kuwa tupo sehemu 1 ya kutafuta njia ya kufika sehemu husika…..pia napenda kuwapa pole kwa wale wooote walio patwa na matatizo siku kama ya leo, Haswa ndugu zetu waliopo mahospitalini….pia napenda kuwapongeza rafiki zangu woooote akiwepo ADILI MKWELA NA WILIAM ELISA,MKOLONI,DANI, EMAX, BONNY JONII SULTAN WATU WA REDIO NA WATU WA BLOGS,WEB NA MASHABIKI WOOTE WA MUZIKI WA RAMA DEE NK! ….siku yangu ya kuzaliwa ipo na matukio mengi sana siwezi kuyasema yote ila kikubwa TUWE NA SUBIRA KATIKA MAAMUZI YA KIMAISHA ILI TUSIJE KUSUMBUA WATU MBELE YA SAFARI #MIZINGA .Thanks all friends so ntasikia poa kama wooote mtasema HAPPY BIRTHDAY RAMA DEEEE………...
0 comments:
Chapisha Maoni