Alhamisi, Julai 03, 2014

CHANZO CHA KUCHAKAA HARAKA KWA NOTI YA TSH. 500

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema sababu ya noti ya  sh. 500 kuchakaa mapema ni kutokana na kutumika na watu wengi wasio na mzunguko wa huduma za kibenki.
Akizungumza katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba), Ofisa wa BoT, Abdul Dollah, alisema noti zote zinatengenezwa kwa malighafi ya aina moja, lakini kinachotokea ni noti ya sh. 500 kutumika kupita kiasi.
Ni asilimia 14 ya Watanzania ndio wanatumia huduma za kibenki, waliosalia hawatumii, sasa ukija katika noti za sh. 500 na 1,000, zinachoka sana maana ndizo zinazoshikwa na watu wengi wa tabaka la kawaida,
alisema.
Aliwataka wale wenye noti zilichokaa kuzirudisha BoT, ili wapatiwe noti mpya.

0 comments:

Chapisha Maoni