Meneja mpya wa Manchester United Louis van Gaal ameambiwa kuwa anaweza
kutumia kiasi chochote cha fedha kusajili wachezaji wapya Old Trafford
na hata kuvunja rekodi za uhamisho (Guardian), Man U Pia wametajiwa kuwa
wanaweza kuendelea kumsaka Angel Di Maria, 26, kufuatia Real Madrid
kumsajili kiungo mshambuliaji James Rodriguez, 23, kutoka Monaco
(Independent), Arsenal wamekubali ada ya uhamisho ya pauni milioni 3
kumsajili kipa wa David Ospina, 25 kutoka Nice ya
Ufaransa (Guardian), boss wa Liverpool Brendan Rodgers anataka
kumsajili beki wa kulia Javier Manquillo, 20, kutoka Atletico Madrid kwa
mkopo. Mchezaji huyo anawindwa pia na Arsenal (Sun), Atletico Madrid
wanawanyatia wachezaji wawili wa Arsenal, Santi Cazorla na Nancho
Monreal (Daily Telegraph), Arsenal wamerejea kumyatia kiungo wa Sporting
Lisbon William Carvalho, 22, baada ya mazungumzo ya kumchukua Sami
Khedira wa Real Madrid, 27, kusuasua (Daily Star), Tottenham na Arsenal
wanaonesha nia ya kumsajili kiungo mshabuliaji Douglas Costa, 23, kutoka
Shakhtar Donetsk. Mchezaji huyo kutoka Brazil amekataa kurejea Ukraine
kutokana na matatizo ya kisiasa katika nchi hiyo (Independent),
mshambuliaji Divock Origi, 19, amesafiri kwenda Marekani kukamilisha
usajili wake wa Liverpool, lakini atabakia Lille kwa msimu ujao (Daily
Express), uwezekano wa Didier Drogba, 36, kurejea Chelsea huenda
kukasababisha Romelu Lukaku kuondoka Darajani, na huenda akaenda Everton
(Daily Telegraph), Everton wameripotiwa kukaribia kumsajili David
Henen, 18, kutoka Anderlecht (Liverpool Echo), Inter Milan wako makini
kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez, baada ya
kuambiwa na Manchester City kuwa Stevan Jovetic, 24, hauzwi (Sun), Hull
City wanazungumza na beki wa kimataifa kutoka Cameroon Jean-Armel
Kana-Biyik, 25 kutaka kumsajili kutoka Rennes ya Ufaransa (Sky Sports),
Lionel Messi, 27, 'alitishia' kujiunga na Arsenal msimu uliopita, wakati
akizungumzia mkataba wake mpya na Barcelona (Daily Mail), Luis Suarez,
27, ameukimbia mji wa Barcelona, kuwaepuka waandishi wa habari
wanaomfuatilia kwa karibu (Daily Star), Manchester United wanajiandaa
kutoa pauni milioni 39 kumchukua Arturo Vidal, 27, kutoka Juventus
(Tuttosport), klabu ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani imefuta
mazungumzo na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Nicklas Bendtner, 26,
kwa sababu mchezaji huyo anataka mshahara mkubwa (Le Figaro), meneja wa
Borussia Dortmund Jurgen Klopp ametupilia mbali tetesi kuwa beki Mats
Hummels, 25, anakwenda Manchester United, na kiungo Marco Reus, 25
anakwenda Bayern Munich (Bild), Atletico Madrid wanashindwa kutoa pauni
milioni 13 wanazotaka Chelsea kumsajili Fernando Torres, 30, licha ya
kuwa meneja Diego Simione kutaka sana kumchukua (AS).




0 comments:
Chapisha Maoni