Kiasi cha wanafunzi 100 wa shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani
Monduli wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao
kuteketea na moto leo(Jumatano) asubuhi.
Moto huo ambao inaelezwa
chanzo chake ni hitilafu ya umeme ilitokea wakati wanafunzi wote wako
darasani. Hakuna mtu yoyote aliyedhurika lakini mali kadhaa za wanafunzi
zimeteketea.
Kikosi Cha zimamoto kutoka Arusha kulifikisha wakati tayari mabweni hayo yameshateketea.
Edward Lowasa kama Mbunge wa Monduli ametembelea shule hiyo na kuwaahidi
kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati utaratibu unafanywa
kurejesha katika hali ya kawaida. Gharama za kuwasafirisha ni shilingi
laki Saba.
Aidha Lowasa kama mbunge wa Monduli kwa kushirikiana na
kiwanda Cha magodoro Cha Tanform Cha Arusha kimetoa msaada wa magodoro
100 kufuatia kadhia hiyo.





0 comments:
Chapisha Maoni