Watu wenye silaha wameishambulia kambi moja ya kijeshi huko
mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lambert Mende msemaji wa
serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameeleza kuwa kundi la
watu wenye silaha jana liliishambulia kambi ya jeshi la Tshatsi huko
Kinshasa mji mkuu wa nchi hiyo.
Mende amesema kuwa wavamizi hao waliokuwa na lengo la kuingia katika kambi hiyo ya kijeshi, hata hivyo waligonga mwamba.
Baadhi ya duru za habari zinasema kuwa jeshi la Kongo lilifanikiwa kuwauwa wavamizi kadhaa katika shambulio hilo.
Kambi ya kijeshi ya Tshatsi huko Kinshasa iliwahi kushambuliwa pia mwezi Disemba mwaka jana.




0 comments:
Chapisha Maoni