Jumanne, Julai 22, 2014

BONGE LA BIFU, SHILOLE VS BABY MADAHA

Ugomvi mzito umeibuka kati ya mastaa wa Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Baby Madaha baada ya kurushiana vijembe.
Baby Madaha aliwahi kunukuliwa akisema kuwa Mwezi wa Ramadhani unambana kiuchumi, kwa vile kumbi nyingi za starehe zimefungwa, hivyo anakosa shoo.
Lakini kwa upande mwingine yeye Shilole amesema anamshangaa Madaha kwa kukosa hofu ya Mungu, huku akimchana kuwa, haweki akiba, anaishi maisha ya kutegemea shoo ndiyo maana anaulalamikia mwezi huu.
Madaha alivyoelezwa kuhusu maoni ya Shilole, alikuja juu na kutema cheche:
Shilole anatafuta kiki kupitia jina langu, kwanza si hadhi yangu. Siwezi kujibishana na msanii anayetegemea shoo za kwenye vigodoro, akatafute pa kutokea.

0 comments:

Chapisha Maoni