Kiungo wa Juventus Arturo Vidal ameipa pigo Manchester United kwa kudai
hatokwenda Old Trafford (Daily Mail), Liverpool watatumia madai hayo
kumfuatilia kwa makini Vidal kwa kutoa pauni milioni 42.5 (Metro),
Atlètico Madrid wameanza kumfuatilia mshambuliaji wa Manchester United
Javier Hernandez, 26 (Times), kiungo wa Chelsea Marko Marin, 25,
anazungumza na Besitkas kwenda kwa mkopo (Sun), meneja wa Aston Villa,,
Paul Lambert amesema nahodha wake Ron Vlaar,
29, anayefuatiliwa na Tottenham, hauzwi (Sun), beki wa Spurs Vlad
Chiriches huenda akaenda Roma (Sun), Jose Mourinho anakaribia
kukamilisha uhamisho wa Didier Drogba, 36, huku kipa Petr Cech, 32,
akimuonya Mourinho kutomkalisha bench msimu ujao (Sun), Arsenal
wanamfuatilia kipa wa Real Madrid Iker Casillas, 33, na wamempa mkataba
wa miaka mitano kwa mshahara wa pauni milioni 1.4 kwa mwaka (Daily
Express), Manchester United wanapanga kumfuatilia Memphis Depay, 20 wa
Uholanzi (Sun), Per Mertesacker, 29, Mesut Ozil, 25 na Lukas Podolski,
29, watakosa mwanzo wa msimu baada ya kuongezewa likizo kufuatia
kushinda Kombe la Dunia (Daily Mirror), Ryan Giggs amemuelezea meneja
mpya wa Manchester United Louis van Gaal, kama "Alex Ferguson Mpya"
(Telegraph), nahodha wa Liverpool Steven Gerrard, 34, anajiandaa kusaini
mkataba wa mwaka moja zaidi (Liverpool Echo), Inter Milan imedai
inakaribia kumsajili beki Gary Medel wa Cardiff City (Wales Online),
Sunderland wana matumaini ya kumsajili beki wa Chelsea Patrick van
Aanhold (Metro), Arsenal wanamtazama kwa karibu Douglas Costa ambaye
amekataa kurudi Shakhtar Donetsk kutokana na matatizo ya kisiasa.
Mchezaji huyo anafuatiliwa pia na AC Milan na Spurs (Sky Sport Italia),
Arsenal wanajiandaa kuwasilisha maombi yao kwa Hoffenheim kumsajili
Roberto Firmino. Mshambuliaji huyo kutoka Brazil anatakiwa pia na Inter
Milan (Tuttomercatoweb.com) matumaini ya Manchester United kumsajili
Juan Cuadrado yameongezeka baada ya Bayern Munich kuacha kumfuatilia
mchezaji huyo wa Fiorentina (talkSPORT)
0 comments:
Chapisha Maoni