Wanachama wa mfuko wa hifadhi ya
jamii NSSF mkoa wa Kilimanjaro wamelalamikia kero ya usumbufu na lugha
ambazo siyo nzuri zinazotolewa na wafanyakazi wa mfuko huo kwa wanachama
pindi wanapodai mafao yao.
Hayo yamebainishwa na mwakilishi wa wafanyakazi wa serikali kuu na
afya tughe mkoa wa Kilimanjaro Bi Gresta Sodaka wakati wa tume
iliyoundwa kuchunguza kero za wanachama wa mfuko huo ilipokuwa
inawakiilisha malalamiko hayo kwa meneja wa mfuko wa hifadhi ya jamii
mkoani Kilimanjaro.
Amesema kero zinazowakabili wanachama ni nyingi ikiwemo waajiri
kutowasilisha michango ya wanachama na pindi wafanyakazi wanapostaafu na
kufuatailia mafao yao kujikuta wanapata mafao kidogo ambayo hayalingani
na muda waliofanya kazi.
Kwa upande wake katibu wa chama cha wafanyakazi wa serikali kuu na
afya tughe mkoa wa Kilimanjaro Bw. Simon Msuya ameiomba serikali
kusimamia mifuko ya jamii ili iweze kutoa mafao yanayolingana kwa
wananchama wote wanaojiunga na mifuko hiyo hapa nchini.
Akijibu malalamiko hayo meneja wa mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF
mkoa wa Kilimanjaro Bi Delifina Masika amesema haweza kukubali wala
kukataa malalamiko yaliyotolewa dhidi ya wafanyakazi wa mfuko huo na
kuahidi kufuatilia ili kutokomeza kero hizo ambazo hazistahili kwa kuwa
kufanya hivyo ni kinyume na taratibu za mfuko huo.
0 comments:
Chapisha Maoni