Vijana wa kike wenye vipaji vya fani ya muziki wamelalamika kupata
vikwazo na usumbufu mkubwa wanapotaka kutumia fani yao kujitolea
kusaidia jamii hali inayowakatisha tamaa na wameziomba idara
zinazohusika kuwasaidia kuondoa changamoto hizo.
Mmoja wa vijana hao Bi. Lidiya Mchaina amesema licha ya tatizo hilo
kuwaathiri vijana wote ni kubwa zaidi kwa vijana wa kike na linahitaji
kudhibitiwa kwani licha ya kukwamisha jitihada za vijana wa kike za
kujinasua na utegemezi na pia umaskini ni unyanyasaji wa kijinsia.
Akizungumzia malalamiko hayo mmbunge wa jimbo la Arusha Mh Godbless
Lema ambaye amekutana na baadhi ya vijana hao amesema atafuatilia na
amewataka kutokata tamaa na kwani hakuna kisichowezekana na pia
wasichoke kutoa taarifa za changamoto zinazowakabili kwani hakuna
kilicho rahisi.
0 comments:
Chapisha Maoni