Tarehe 25 Julai mwaka 1938 Wapalestina wasio na hatia 62 waliuawa na
mamia ya wengine kujeruhiwa katika milipuko miwili ya mabomu iliyotokea
kwa nyakati tofauti katika soko la kuuzia mboga za majani huko
Palestina. Makundi ya kigaidi ya Wazayuni ndiyo yaliyotega mabomu hayo
mawili na lengo lao lilikuwa ni kuzusha hali ya machafuko na ukosefu wa
amani kwa Wapalestina. Wazayuni wamekuwa wakizusha hali ya wasiwasi na
vitisho kwa wananchi wa Palestina kwa kushambulia vijiji na maeneo yenye
watu wengi katika miji mbalimbali ya Palestina pamoja na kuwauwa
shahidi raia wasio na ulinzi, jinai ambazo zinaendelea hadi sasa.
0 comments:
Chapisha Maoni