Mtu mmoja amefariki Mkoani Iringa baada ya kugongwa na gari huku jeshi la polisi likimtafuta mtu mmoja kwa tuhuma za kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka minne.
Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema Rodi Kindole mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa kijiji cha Ilula wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa amefariki baada ya kugongwa kwa gari no.T:377 CAX aina ya Yutong Bus mali ya kampuni ya Super Feo.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa ajali hiyo imetokea kijiji cha Mazombe barabara kuu ya Iringa-Morogoro na gari hilo lilikuwa linaendeshwa na dereva Godfrey Chengula umri miaka 37 ambapo uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa akiendesha baiskeli huku akiwa amelewa.
Wakati huo huo amesema jeshi la polisi Mkoani Iringa linamtafuta mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Cosmas mkazi wa eneo la Mkwawa Manispaa ya Iringa kwa tuhuma ya kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka minne na kumsabishia maumivu makali.
Aidha amesema chanzo cha tukio hilo ni tamaa ya mapenzi ambapo mtuhumiwa ametenda kosa hilo wakati mtoto huyo akiwa anacheza jilani na nyumba yao.
Hata hivyo Kamanda Mungi ameongeza kuwa askali polisi Wakiwa doria wamemkamata Chiku Husseni mwenye umri wa miaka 50 mkazi wa eneo la Mshindo Manispaa ya Iringa akiwa na mtambo pamoja na vifaa mbalimbali vya kutengenezea pombe aina ya gongo ambapo chajo chake ni kujitafutia kipato.

0 comments:
Chapisha Maoni