Alhamisi, Julai 24, 2014

TANZANIA ILIVYO MEREMETA KATIKA SHEREHE ZA UFUNGUZI WA MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA

Jina la Tanzania linameremeta wakati wanamichezo wetu walipopita katika maandamano ya ufunguzi wa Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye sherehe kabambe za ufunguzi katika Uwanja wa Celtic Park jijini Glasgow, Scotland, uliobeba watazamaji 40,000 huku watu bilioni 1 wakiangalia live sherehe hizo kupitia katika TV zao. Takriban  mashabiki 100,000, na wanamichezo 4,000 kutoka katika nchi 71 zitakazoshindana wapo hapo kwa michezo hiyo ambapo hii ni mara ya 20 kufanyika toka ianzishwe. 
Nahodha na bondia wa Tanzania Seleman Salum Kidunda akipeperusha juu bendera ya Taifa wakati akiongoza wenzake kwenye maandamano hayo ya ufunguzi 





0 comments:

Chapisha Maoni