Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) umetangaza kukipeleka kwenye
matengenezo makubwa kivuko cha Mv Kigamboni, kinachotoa huduma ya
kuvusha watu na magari kwenda na kurudi Kigamboni jijini Dar es salaam.
Aidha huduma za uvushaji watu pamoja na magari zitaendelea kutolewa
na vivuko vya Mv Magogoni pamoja na Mv Lami katika kipindi chote cha
matengenezo husika.
Ofisa Habari wa Temesa, Theresia Mwami alimwambia mwandishi jana kuwa
wakala huo unaomba radhi kwa usumbufu ambao wananchi wanaotumia vivuko
watakaoupata wakati kivuko hicho kitakapokuwa kwenye matengenezo.
wami alisema vivuko hivyo havijafanyiwa matengenezo makubwa kwa muda
mrefu hivyo kitafanyiwa matengenezo kivuko cha Mv Kigamboni kwanza na
baadae Mv Magogoni.
Alisema kivuko cha Mv Lami kina uwezo wa kuchukua abiria 100 na
magari madogo 16 wakati kivuko cha Mv Kigamboni kinachukua magari 23 na
abiria 800.
0 comments:
Chapisha Maoni