Jumatano, Julai 09, 2014

TAARIFA KAMILI YA KIFO CHA MMILIKI NA MKURUGENZI WA SWEET FM NA SWEET TV, EMMANUEL MBUZA

Mmiliki na mkurugenzi wa Sweet Fm radio ya mkoani Mbeya na Sweet Television, Emmanuel Mbuza amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Tumbi alikokuwa akitibiwa baada ya kuugua kwa wiki mbili mfululizo.
Taarifa za uhakika toka kwa meneja wa Sweet fm, Yohana Mwambene zinaeleza kuwa Mbuza ambaye pia alikuwa ni katibu mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Mbeya mjini alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari kilichompata ghafla pamoja na shinikizo la damu, magonjwa yaiyomfanya awe na hali mbaya iliyopelekea kifo chake katika hospitali ya Tumbi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwaajili ya matibabu.
Emmanuel Mbuza (Mzaliwa wa mbeya aliyekua anafanya biashara zake jijini Dar es salaam.) ni mhitimu wa sangu High school(2007), aliewahi kua Mfanyakazi wa Mbeya FM na generation FM, na msomi wa Masters ya sheria aliyoichukua katika chuo kikuu cha Tumain cha Iringa.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kesho alhamisi kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Mbeya ambako shughuli za mazishi zinatarajiwa kufanyika katika makaburi ya ukoo maeneo ya kalobe jijini Mbeya, lakini kwa sasa msiba Tabata jijini Dar es Salaam na Ilemi-Juhudi Mkoani Mbeya. BWANA ametoa, BWANA ametwaa, jina lake lihimidiwe...AMEN

0 comments:

Chapisha Maoni