Kufuatia kushamiri kwa matukio ya watu kufanya matukio ya uhalifu kwa
kutumia mabomu jeshi la polisi limesema litahakikisha linauteketeza
mtandao wa watu hao wanaojihusisha na vitendo hivyo ambapo mpaka sasa
zaidi ya watu 25 wanashikiliwa kwa nchi nzima kutokana na kujihusisha
na matukio hayo.
Kufuatia kushamiri kwa matukio ya watu kufanya
matukio ya uhalifu kwa kutumia mabomu jeshi la polisi limesema
litahakisha linauteketeza mtandao wa watu hao wanaojihusisha na vitendo
hivyo ambapo mpaka sasa zaidi ya watu 25 wanashikiliwa kwa nchi nzima
kutokana na kujihusisha na matukio hayo.
Akizungumza jijini dar es salaam mkurugenzi wa
upelelezi wa makosa ya jinai isaya mngulu amesema siyo kwamba jeshi la
polisi limeshindwa kupambana na matukio hayo ila kazi bado inaendelea
japo wananchi wanapaswa kutoa taarifa kwa kila jambo wanaloona halipo
sawa.
Chanzo kilitembelea katika taasisi ya mifupa moi na
kufanikiwa kuzungumza na msemaji wa taasisi hiyo bw almas juma kuhusu
hali ya majerui wawili waliolazwa katika hosptal hiyo wakitokea Arusha
kufuatia kulipuliwa kwa bomu wakiwa katika futari amesema ali zao
zinaendele vyema.
Aidha ilifanikiwa kuzungumza na majeruhi hao
sheikh Soud Ally Soud na sheikh Muhaji Hussein ambao wanaelezea hali
ilivyo kuwa huku wakiliomba jeshi la polisi kulishughulikia kwa kina
jambo hilo.




0 comments:
Chapisha Maoni