Jumanne, Julai 22, 2014

REAL MADRID WAMSAJILI JAMES RODRIGUEZ

Real Madrid wamemsajili mshindi wa kiatu cha Dhahabu katika michuano ya Kombe la Dunia Brazil 2014, James Rodriguez.
Mshambuliaji huyo kutoka Colombia mwenye umri wa miaka 23 amesaini mkataba wa miaka sita na Real Madrid akitokea Monaco.
Imeripotiwa ada yake ni takriban pauni milioni 63 na kumfanya mchezaji wa nne wa uhamisho wa gharama, nyuma ya Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez.
Rodriguez alifunga magoli sita katika mechi tano za Kombe la Dunia, wakati timu yake ilipofika katika robo fainali.
Pichani James Rodriguez akiwa katika vipimo vya afya Real Madrid.

0 comments:

Chapisha Maoni