Jumanne, Julai 22, 2014

MAGAIDI WA MABOMU NATINDIKALI WAMEKAMATWA ARUSHA

JESHI la Polisi jijini Arusha limewakamata watu 16 akiwemo Imam wa Msikiti wa Al Quba uliopo mkoani Arusha, Jafar Lema na mfanyabiashara 1 wote wakihusishwa na matukio ya ulipuaji wa mabomu jijini Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai nchini (DCI), Issaya Mungulu, katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Arusha leo, Jumanne Julai 22, 2014 imedaiwa kuwa Julai 21, 2014 saa 20.00 usiku katika maeneo ya Sombetini, Jeshi hilo limewakamata Yusufu Ally (30) na mkewe Sumaiya Juma (19) wakiwa nyumbani kwao baada ya kupekuliwa walikutwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono Saba (7), risasi sita za bunduki aina ya shortgun, mapanga mawili, unga wa baruti unaokadiriwa kufika nusu kilo na bisibisi moja.
Mungulu amenukuliwa na FiCHU0 akisema kuwa Yusufu ni miongini mwa watuhumiwa waliokuwa wanatafutwa kwa ulipuaji wa mabomu maeneo yote jijini Arusha na kuwa mahojiano juu ya mtuhumiwa bado yanaendelea dhidi yake.
Aidha, amesema uchunguzi wa shauri hilo pamoja na matukio mengine ya milipuko yanaendelea ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa walioko mikononi mwa polisi na kuwakamata watakaobainika kuhusika na matukio hayo.

0 comments:

Chapisha Maoni