Serikali imeahidi kushirikiana na viongozi wa dini ili kuhakikisha amani endelevu nchini na kupata maendeleo ya wananchi wake.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda amesema kwa niaba ya Rais, kwenye sherehe ya jubilee ya miaka 25 ya uaskofu iliyofanyika Mkoani Iringa , kuwa kiongozi makini ni yule anayekubali kukosolewa na kurekebisha mapungufu na kuahidi kuchukua hatua stahiki kwa yote wanayoshauriwa.
Mhe. Pinda amezungumzia suala la rasimu kuwa ni vema wananchi wakaacha wabunge waboreshe katika maeneo yenye mapungufu kwa ajili ya manufaa ya wananchi
Aidha, amewakumbusa wabunge wenye dhamana ya kupitia rasimu kurejea bungeni ili kujenga hoja za kuboresha mapungufu kwenye kufikia uamuzi wa mwisho wa kupatikana katiba hiyo ambapo wananchi wenyewe ndiyo waamuzi wa kura ya maoni.
Hata hivyo, Mhe. Pinda ametoa wito kwa viongozi wa dini na maaskofu kuombea uchaguzi wa serikali za mitaa na chaguzi nyingine za mwakani ili kuweza kupata viongoizi waadilifu.

0 comments:
Chapisha Maoni