Alhamisi, Julai 24, 2014

NDEGE YA ALGERIA ILIYOPOTEA JANA IMEANGUKA NA KUUA ABIRIA 110

Kanali ya televisheni ya al Nahar ya Algeria imetangaza kuwa abiria 110 na wahudumu sita wamepoteza maisha katika ajali ya ndege iliyotokea jana.
 Kwa mujibu wa kanali hiyo, ajali hiyo imeihusisha ndege ya shirika la ndege la Algeria na kwamba imetokea muda mchache baada ya ndege hiyo kuruka kutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ouagadougou mji mkuu wa Burkina Faso. Imeelezwa kuwa awali ndege hiyo ya abiria, ilipoteza mawasiliano na shirika la anga la Algeria kwa muda wa saa moja baada tu ya kuvuka anga ya Niamey, mji mkuu wa Niger kabla ya kuanguka. Ndege hiyo ni Airbus 320, yenye namba za usajili EH5017. Kanali ya televisheni ya al-Nahar imetangaza kuwa, wahudumu wa ndege hiyo waliokuwa raia wa Uhispania nao wamefariki dunia na hivyo kuifanya idadi ya wahanga wa ajali hiyo kufikia 116 na kwamba, ndege hiyo ilikuwa imekodishwa kutoka shirika la ndege la Uhispania. 
Aidha imeeelezwa kuwa ndege hiyo haikuwa na hali nzuri ya kuruka ambapo hata kabla ya mwezi huu wa Ramadhani, ilikuwa ikifanyiwa matengenezo. Waziri wa Usafirishaji nchini Ufaransa, Frédéric Cuvillier amesema kuwa, asilimia kubwa ya abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo, walikuwa raia wa Ufaransa.

0 comments:

Chapisha Maoni