Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt.Christine Ishengoma kuongoza maadhimisho ya
siku ya mashujaa leo July 25 katika kijiji cha lugalo wilaya ya kilolo
MKoa wa Iringa.
Afisa wa habari wa MKuu wa Mkoa wa Iringa Bw.Denis Gondwe amesema maadhimisho hayo yatafanyika katika kaburi la Nyundo ambaye ni mmoja wa mashujaa waliofariki wakiwa katika harakati za kupigania uhuru kipindi cha ukoloni.
Bw.Gondwe ameongeza kuwa maadhimisho hayo yataenda sambamba na gwalide kutoka jeshi la polisi Mkoani Iringa pamoja na uwekaji wa mashada na silaha mbalimbali za kale ikiwa ni pamoja mishale,upinde na shoka katika kabuli hilo.
Aidha amesema licha ya kufanyika kwa shughuli hizo kutakuwa na viongozi wa kutoka dini na madhehebu mbalimbali ambao wataongoza maombi ya kuombea amani ya taifa letu kwa ujumla.
Hata hivyo ametoa wito kwa wakazi wa wilaya ya KIlolo na MKoa kwa ujumla kujitokeza katika maadhimisho hayo ili kuonesha upendo kwa mashujaa waliofia taifa letu katika kutukomboa kutoka utawala wa kikoloni.

0 comments:
Chapisha Maoni