Jumanne, Julai 29, 2014

MUHIMU KWAKO UNAYEPENDA UREMBO WA KUCHA

Kucha kwa wanawake ni eneo lingine linolatakiwa kuwekwa katika unadhifu. Kuna baadhi ya wanawake unaweza kukutana nao kucha zao zimelika aidha kwa kung'atwa au kwa kuliwa na fangasi. 
Ipo aina fulani ya fangasi ya kwenye kucha inawashamblia san wanawake hususan kwa mkoani Dar, sijui ni kutokana na maji kwa sababu ya kufua au kuosha vyombo au kitu kingine. 
Ni vyema wanawake wenye tatizo hilo kumuona tabibu mtaalamu wa ngozi kwa msaada wa tiba. Unaweza kukutana na mwanamke kucha zake zimelika na zina sharp edges kiasi kwamba akikugusa utadhani umeguswa na msasa. 
Au akishika Glasi ya Kinywaji ukiangalia kucha utadhani mkono ni wa mwanaume maana kwa jinsi kucha zake zilivyo hata hafanani nazo. Kuna kucha za bandia kama mwanamke ana matatizo ya kucha basi akazinunue kusitiri aibu.

0 comments:

Chapisha Maoni