Wasanii wa Tanzania wenye mashabiki wengi Afrika Mashariki,
Lady Jay Dee na Diamond Platinumz, wameitoa Tanzania Kimasomaso kwa
kushinda tuzo moja moja katika tuzo za AFRIMA (African Muzik Magazine
Awards 2014), zilizofanyika jana Dallas, Marekani.
Kwa mujibu wa mtandao wa African Music Magazine, Lady Jay Dee
alishinda tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa Afrika Mashariki na Diamond
Platinumz alishinda tuzo ya Msanii bora wa kiume wa Afrika Mashariki.
Hata hivyo, kwa habari ambazo zimeenea Tanzania na kutajwa kuwa
zilizotolewa na meneja wa Diamond zinaeleza kuwa Diamond ameshinda tuzo
mbili ambayo nyingine ni wimbo bora wa kushirikiaha.
Lakini kwenye orodha halisi ya mtandao a AFRIMMA, tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana imeenda kwa Mafikizolo feat Uhuru (Khona).
Kwa mujibu wa maelezo aliyoandika Diamond kwenye Instagram, inaonesha kama ameshinda tuzo zaidi ya moja.
“First of all napenda nimshkuru sana Mwenyez mungu, Mama, Family, My
management, kipenzi changu, Media, bila kuwasahau nyinyi mashabiki zangu
pendwa kwani sikuzote mmekuwa mkinisupport bega kwa bega kwenye shida
na raha...Niwashkuru pia Wasanii wenzangu toka nje na ndani ya Tanzania
kwani naamini changamoto tunazopeana ndio zimefanya hadi sasa mziki wetu
ufikie hapa...hakika tunzo hizi si zangu bali ni za Muziki wa Bongo
flavour... Mwisho kabisa nimshkuru Mh Rais Jakaya Mrisho kikwete kwa
mchango wake wa kila siku katika sanaa yetu!... Mr President your Son
Did it!!!!! #MdogMdogo.”
Hii ni orodha kamili ya washindi wa AFRIMMA 2014
Best DJ Africa 2014- Dj Black (Ghana)
Best African DJ USA 2014 – Dj Josh (Kenya)
Best Video of the Year 2014- Flavour (Nigeria)
Best Male East Africa 2014- Diamond (Tanzania)
Best Male West Africa 2014- Davido (Nigeria)
Best Female East Africa 2014- Lady Jaydee (Tanzania)
Best Female West Africa 2014 – Tiwa Savage (Nigeria)
Best Male Central Africa 2014 – Fally Pupa (Congo)
Best Female Central Africa 2014- Gasha ( Cameroon)
Best Male Southern Africa 2014- Khuli Chana (South Africa)
Best African Group 2014- P-square (Nigeria)
Best Male Diaspora 2014- Fuse ODG (Ghana)
Best Female Diaspora 2014- Les Nubians (Cameroon)
Best Female Southern Africa 2014- Zahara (South Africa)
Best Dancehall Artist 2014 – Timaya (Nigeria)
Best Dance in a Video 2014- Iyanya (Lekwa Ukwu) (Nigeria)
Best Gospel Artiste 2014- Bahati (Kenya)
Best Traditional Artist 2014- Flavour (Nigeria)
Best Newcomer 2014- Stanley Enow (Cameroon)
Best Video Director 2014- Ogopa Dj’s (Kenya)
Music Producer of the year 2014- Dj Oskido (South Africa)
Best Dance Group 2014- Imagineto (Nigeria)
Best Rap Act 2014- Sarkodie (Ghana)
Best Collaboration 2014- Mafikizolo ft Uhuru (Khona) (South Africa)
Song of the Year 2014- Kcee (Nigeria)
Artist of the Year 2014- Davido (Nigeria)
Leadership in Music Award 2014- 2face Idibia
Legendary Award 2014- Yvonne Chaka Chaka
Transformational Leadership Award 2014- Chief Dr. Godswill Akpabio
0 comments:
Chapisha Maoni