Jumapili, Julai 27, 2014

TAARIFA YA KIFO CHA MCHEKESHAJI NGULI WA TV

Mchekeshaji/muigizaji maarufu wa kipindi cha Mashtaka kinachorushwa na Citizen TV, Nancy ‘Jastorina’ Nyambura amefariki Jumamosi (July 26).
Kwa mujibu wa Citizen TV, Jastorina alikuwa anaumwa muda mrefu ugonjwa wa ‘Meningitis’ na alikuwa akipata matibabu katika hospitali ya Kenyatta nchini humo.
Jastorina ambaye mwaka huu alishinda tuzo ya Kalasha kama msanii bora wa Ucheshi (Comedy), ameacha watoto wawili wa kiume.
Apumzike kwa Amani. Amina!

0 comments:

Chapisha Maoni