Jumapili, Julai 27, 2014

BAHATI BUKUKU AVUNJIKA KIUNO KATIKA AJALI, IMESHINDIKANA KUHAMIA DAR ES SALAAM

Muimbaji wa nyimbo za injiri Bahati Bukuku amapata ajali ya gari akiwa na dereva wake, Eddy maeneo ya Kongwa Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Akiongea kwa simu Bahati amesema: 
Ni Mungu tu aliyetuokoa, tulikuwa tunaelekea Kahama kwenye huduma ghafla tukagongana uso kwa uso na lori, gari yetu aina ya Toyota Nadia iliruka na kubiringika kama mara tatu hivi, tumetoka tukiwa tumeumia sana.
Hapa siwezi kusimama wala kukaa na dereva wangu kaumia sana mguu. Gari yangu imeumia sana wala huwezi kuamini kama kuna mtu katoka salama. 
Watu mbalimbali wamefika hospitali kumtazama Bahati Bukuku akiwemo rafiki yake Jennifer Mgendi hospitalini kongwa mkoani dodoma alikolazwa baada ya kupata ajali ya gari. Juhudi za kumwamishia hospitali ya taifa muhimbili zimeshindikana!

0 comments:

Chapisha Maoni