West Ham wanataka kumsajili mshambuliaji wa
Cameroon, Samuel Eto'o, 33 ambaye aliondoka Chelsea msimu uliopita (Sun
on Sunday), Inter Milan wanafikiria kumtoa Fredy Guarin, 28,
kubadilishana na Javier Hernandez, 26, kutoka
Manchester United (Sun on Sunday), Romelu Lukaku aliyecheza Everton kwa
mkopo msimu uliopita, anataka uhamisho wa kudumu kwenda Goodison Park
(Talksport), Arsenal wanakaribia kukamilisha uhamisho wa kiungo wa
Shakhtar Donetsk, Douglas Costa, 23 ambaye ameomba kuondoka Ukraine kwa
sababu za matatizo ya kisiasa nchini humo (Caughtoffside), Atlètico
Madrid wamefikia makubaliano ya kumsajili Antoine Griezmann, 23 kutoka
Real Sociedad kwa pauni milioni 24 (AS), meneja wa. Manchester United
bado ana nia ya kumsajili kiungo wa Roma Kevin Strootman, 24, licha ya
mchezaji huyo kuwa majeruhi kutokana na kuumia goti (Sky Sports), Real
Madrid wanapanga kumchukua Radamel Falcao, 28, kwa mkopo na uhamisho wa
kudumu mwaka 2015 (AS), jaribio la Stoke City kumsajili Oussama Assaidi,
25, kutoka Liverpool kwa pauni milioni 7, huenda likashindikana
kutokana na winga huyo kutaka mshahara mkubwa (Daily Express),
mshambuliaji wa Lille Divock Origi, 19, anakaribia kukamilisha uhamisho
wa pauni milioni 12.5 kwenda Liverpool (Sunday Mirror), Sami Khedira
anataka mshahara wa pauni milioni 7.1 kwa mwaka ili kujiunga na Arsenal
(La Sexta), Arsenal wanafikiria kupanda dau kumchukua kiungo wa
Southampton Morgan Schneiderlin (Daily Star), Angel Di Maria anajiandaa
kusaini mkataba wa miaka mitano siku chache zijazo na Paris St-Germain
(Marca).
0 comments:
Chapisha Maoni