Jumapili, Julai 27, 2014

WANAWAKE WANAOJIREMBA SANA HUWATISHA WANAUME

Imebainika kwamba wanawake wanaojiremba sana usoni kwa rangi za midomo zenye kuonekana sana, na vipodozi vingine vikiwemo vile vya kope za macho, huwatisha wanaume badala ya kuwafurahisha au kuwavutia.
Katika tafiti nyingi zilizofanywa kwenye jamii mbalimbalina hasa mijini imebainika kwamba, wanaume saba kati ya kila kumi hupenda nyuso za wanawake zilizowekwa vipodozi kidogo sana. Wale wanawake ambao nyuso zao zimekolezwa vipodozi vingi badala ya kuwafurahisha au kuwavuta wanaume, huwakera na kuwatisha.
Zaidi ya wanaume 6,800 kati ya 10,000 walioshiriki kwenye tafiti hizi, walikiri kwamba, hupenda nyuso za wanawake ambazo ni safi na nyororo, ambazo hazijakandwa tope la vipodozi.Kuna wanawake ambao hutumia mchanganyiko mkubwa sana wa vipodozi unaofikia aina 20 kwa siku. Nyuso za wanawake hawa zimeelezwa kwamba, huchusha kuliko kuvutia. Tatizo la wanawake kujipodoa sana usoni linatokana na kutojiamini kwa wanawake hao. Wao wanadhani kujipodoa sana, kutawafanya wawavutie wanaume na hiyo itawafanya wasione udhaifu wao kwenye maeneo mengine ya mwili au tabia zao. Jambo ambalo halina ukweli.

0 comments:

Chapisha Maoni