Jumamosi, Julai 26, 2014

VIDEO YA WIMBO MPYA YA NAY WA MITEGO 'MR. NAY' INATISHA!!!

Video mpya Nay wa Mitego, 'Mr Nay' inatisha. Rapper huyo anayefahamika kuwa kufanya mambo yake nje ya 'Kumi na Nane' kama Weusi, yupo nchini Kenya ambako amekamilisha kushoot video ya ngoma yake mpya na muongozaji Kelvin Bosco Jr.
Katika picha ambazo Bongo5 imezipata exclusively kutoka Kenya, rapper huyo anaonekana kushoot video kwenye chumba kinachoonekana kama pamefanyika mauaji ya kimbari huku yeye akiwa amekaa kwenye kiti cha enzi kilichotapakaa damu.
Kunaonekana jacuzzi lililojaa dimbwi la damu na wasichana waliofungwa minyororo kama watumwa wakicheza mbele yake.

0 comments:

Chapisha Maoni