WASANII nyota wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na
Hisan Muya ‘Tino’ hivi karibuni walitiwa mbaroni katika mji wa Kilifi
ulio mbele ya Mombasa nchini Kenya baada ya kukutwa wakipiga picha za
filamu yao bila kuwa na kibali.
Hata hivyo, waigizaji hao baadaye
waliachiwa, ingawa hali ilikuwa ngumu kidogo kwa Tino, ambaye polisi wa
Kenya walidai hakuwa Mtanzania, bali ni raia wa Somalia.
Dude alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema liliwatokea
kutokana na mazoea ya huku nyumbani ambako hufanya shughuli zao za
kupiga picha za filamu zao bila kuhitaji kibali.
Yaani tumepata aibu ya mwaka, kwani tulienda kushuti bila kuomba kibali kutokana na mazoea ya huku kwetu Bongo, tulipekuliwa sisi na gari letu, baada ya hapo kibali kikaletwa nikaachiwa lakini Tino waliendelea kumshikilia wakisema ni Msomali mpaka mkuu wa shirikisho la filamu Mombasa alipokuja kuokoa jahazi, ukweli Kenya hakufai
alisema Dude.
0 comments:
Chapisha Maoni