Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu wawili
wanaoshukiwa kuwa majambazi ambao walikutwa wakiwa na bunduki mbili aina
ya shortgun zikiwa zimekamatwa vitako huku moja ikiwa imefungiwa hirizi
kama kinga ya kuzuia wasikamatwe katika matukio ya uhalifu.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Bw Robert Boaz
amesema, watu hao Ibrahimu Machaku na Laurenti Massawe wamekamatwa
juzi na jana katika oparesheni maalum ya kupambana na matukio ya uhalifu
ambapo pia walifanikiwa kukamata kilo 4.5 za dawa za kulevya aina ya
Cocain kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro.
Kamanda Boaz amewaambia waandishi wa habari kuwa
Massawe ambaye ni mkazi wa Arusha pia alikamatwa akiwa na vitu vya
dhahabu na simu mbili ambavyo aliporwa mfanyabiashara mmoja mjini Moshi
Bw Mehboob Sadiki baada ya kuvunjwa nyumba yake Juni 22.
Amesema, katika oparesheni hiyo polisi walikamata
dawa hizo zikiwa zimetelekezwa na abiria aliyekuwa akisafiri na ndege
kutoka Brazil kupitia Ethiopia, Mombasa hadi kwenye uwanja huo na jeshi
la polisi limeanza kumsaka abiria huyo ambaye alitoweka.
0 comments:
Chapisha Maoni