Wengi walikuwa wanajiuliza kunani, haswa siku Wema Sepetu alipoamua
kunyoa Dongo, huku kila mtu akitoka na story yake mwenyewe kwa mtazamo
tofauti bila hata kujua sababu halisi ya uamuzi wake huo, ila ukweli ni
kwamba, Diva huyu ni moja kati ya wasanii wanaochukua kazi yake very
serious, na hii ndio siku alipoamua kupotezea urembo wake na kuvaa
uhusika wake uliomlazimisha kuchukua hatua hiyo ya kunyoa Upara, Akiwa
anaongea katika nyakati tofauti alisikika akifunguka kuwa, Movie mpya
yake anayoifanya iitwayo Family ndio iliyomfanya anyoe upara, huku
akielezea kuwa ilimbidi kufanya hivyo kutokana na uhusika aliotakiwa
kuvaa, uliokuwa unaelezea mtu mwenye Saratani. Wema ni moja kati ya
wasanii wachache ambao hadi hii leo wana uwezo wa kufanya hivi ili tu
kufikisha maudhui ya story iliyokusudiwa kwa jamii.
0 comments:
Chapisha Maoni