Jumapili, Juni 15, 2014

WASTARA APINGA MASTAA KUAGWA LEADERS

Mkali wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amepinga kitendo cha mastaa wa Bongo kuagwa Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar wanapokutwa na umauti.
Wastara alieleza kwa huzuni kubwa kuwa hafurahii eneo la Leaders kutumika kuagia kwa sababu ni eneo hilohilo ambalo hutumiwa kwa starehe.
Ukweli kwa upande wangu napinga mastaa kuagwa Leaders kwa sababu Leaders mara nyingi hutumika kama sehemu ya anasa.Ningeiomba serikali itutafutie sehemu maalum kwa ajili ya kufanyia shughuli zote za misiba ya watu maarufu
alisema Wastara.

0 comments:

Chapisha Maoni