‘’MATESO basi, damu ya Yesu yatosha’’. Hiyo ni kaulimbiu
iliyotolewa katika Kanisa la Nchi ya Ahadi lililopo Sinza-Kamanyola
jijini Dar, chini ya Mchungaji Kiongozi Harris Kapiga, wakati wa maombi
maalumu kwa ajili ya wasanii wa Bongo Muvi ili kuvunja roho ya mauti juu
ya tasnia hiyo ya filamu ambayo imewakumba wasanii wake.
Maombi hayo pia yalikuwa ni kuwaombea ulinzi wote waliomo na wanaotamani kuingia katika tasnia hiyo.
Maombi hayo yaliwakilishwa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania
(TAFF), Saimon Mwakifwamba, wasanii na waimbaji Bahati Bukuku, Dotnata
na wengineo.
0 comments:
Chapisha Maoni