SERIKALI imewataka wanaume kutoona haya na kufika kwenye madawati ya
kijinsia yaliyopo katika vituo vya polisi nchini kutoa taarifa
wanapofanyiwa vitendo vya kikatili na wake zao.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Sophia Simba, alipozungumza na waandishi wa habari
kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Alisema kwa kipindi kirefu wanaume wamekuwa waoga kutoa taarifa pale
wanapofanyiwa vitendo vya kikatili na kuishia kulalamika pembeni na
kuwa wanyonge kwa kuona kuwa wanawake wanapendelewa kuliko wao.
Waziri Simba, aliongeza kuwa ni wakati wa jamii kuendelea kuwa wawazi
na kutoa taarifa mara kwa mara wanapokutana na vitendo hivyo, hasa kwa
watoto, ili viweze kufanyiwa kazi na kuchukuliwa hatua stahiki.
0 comments:
Chapisha Maoni