Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kiislamu
wameshambulia kituo cha polisi na mahoteli na vijiji mjini Mpeketoni,
pwani ya Kenya .
Makabiliano makali yameripotiwa sehemu kubwa ya
Jumapili usiku huku wakaazi wakitorokea maeneo ya msitu karibu na kisiwa
cha Lamu..
Shirika la msalaba mwekundu linasema
kuwa hadi kufikia sasa watu 48 wanahofiwa kuuawa kartika shambulizi
hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo.
Hata hivyo vyombo vya habari vinasema idadi hiyo huenda ikawa juu zaidi.
Shambulizi lilifanyika usiku wa kuamkia leo watu
waliokuwa wamejifunika nyuso zao wakiwa wamejihami vikali walivamia
vituop vya polisi , hoteli na benki.
Shambulizi hilo linakuja siku kadhaa baada ya serikali ya Uingereza kufunga ofisi zake kwa hofu ya usalama.
Duru za jeshi la Kenya zimearifu kuwa wapiganaji hao hawajajitambulisha ni wa kundi gani.
Baadhi ya walioshuhudia wamearifu BBC kuwa
wameona maiti kadhaa na majeruhi wengi japo Polisi hawajathibitisha ni
watu wangapi wameuawa.
Kenya imekumbwa na mashambulio kadhaa kutoka kwa
wapiganaji wa kisomali wa Al Shabaab tangu ipeleke wanajeshi wake ndani
ya Somalia mwaka wa 2011.
Duru kutoka kisiwa cha Lamu zimearifu kuwa
wapiganaji hao walifika katika malori mawili na kurusha kifaa kama bomu
ndani ya kituo cha polisi kisha wakavamia na kuiba silaha.
0 comments:
Chapisha Maoni