Jumatatu, Juni 16, 2014

FIFA 2014 BRAZIL: WAYNE ROONEY ALAUMIWA KWA KUSHINDWA KUFUNGA KATIKA MECHHI YA ITALY

Baada ya Scholes kumtupia madongo Rooney sasa Lejendi wa England na aliyekua nahodha wa taifa hilo Alan Shearer naye amemshutumu Wayne Rooney na kiwango anachoonesha Kombe la Dunia hasa katika mchezo dhidi ya Italy ulioishia kwa kufungwa 2-1.
Shearer alisema:
 Rooney alipata nafasi na akashindwa kuitumia
 alisema. 
Kwenye Kombe la Dunia, labda unapata nafasi moja tu kwenye mchezo na unatakiwa ufunge. Balotelli alipata nafasi moja, goli moja.
Uliona kilichotokea kwa [Arjen] Robben na [Robin] van Persie walipopata nafasi [mchezo wa Netherlands' 5-1 dhidi ya Spain siku ya Ijumaa]. Walifunga. Ndicho unachotakiwa kufanya katika mashindano haya.
Wayne anaweza asipate tena nafasi nzuri kama aliyoipata katika mchezo huu. Anaweza asipate usingizi akiangalia alivyokosa. Nafasi za aina ile unatakiwa kufunga.
Shutma zimekua nyingi kwa Rooney, je unadhani anastahili? vipi kiwango chake unavyokiona katika mchezo uliopita dhidi ya Italy Kombe la Dunia?
Ama unadhani ana kiwango kidogo lakini watu wanatarajia makubwa?

0 comments:

Chapisha Maoni