Jumatatu, Juni 16, 2014

UNADHANI NI SAWA KUMNYONYESHA MTOTO HADHALANI?

Facebook imekuwa ikizua gumzo kuhusu sera na masharti yake ya kuweka picha kwa wanaotumia mtandao huo.
Hivi karibuni, ilikosolewa kwa kuondoa picha ya wapenzi wawili wa jinsia moja wakibusiana , baada ya mtu kusema kuwa picha hizo ni za kukera.
Lakini swala la hivi karibuni ambalo limejadiliwa sana kuhusiana na picha kwenye mtandao huo wa kijamii, ni kuhusu mama mmoja aliyekuwa akimnyonyesha mwanawe hadharani na kuweka picha hiyo kwenye akaunti yake.

Baadhi walisema picha hiyo ilikuwa ya uchi mno na kwamba iliwakera watu wengi sana.
Sasa hivi Facebook imebadilisha sheria zake kuhusu picha za wanawake wakiwanyonyesha watoto wao.
Katika sehemu ya mtandao huo , maagizo sasa yanasema kuwa
Ndio tunaruhusu picha za wanawake wakiwanyonyesha watoto wao ni jambo zuri na ambalo hatuwezi kulikosoa. Ni vyema kujua kuwa ni muhimu kwa akina mama kuonyesha watu picha hizo kwenye Facebook. Picha hizi sasa zinaruhusiwa.
Facebook inasisitiza kuwa mabadiliko yoyote wanayofanyia sera zake kuhusu picha, hutokana na malalamiko ya watumiaji wa mtandao huo.

Katika nchi nyingi za Ulaya, wanawake wengi huogopa kunyonyesha hadharanai kutokana na unyanyapaa. Wanawake nchini Uingereza waliwahi kuandamana wakipinga unyanyapaa unaojitokeza kwa wanawake ambao hunyonyesha watoto wao hadharani.
Swala la kuwanyonyesha watoto hadharani sio hoja kwa wanawake wengi barani Afrika kwani kwao pale ambapo mtoto analilia Titi mama hutafuta mahala safi na kumnyonyeshea mtoto wake.
Nini maoni yako kuhusu swala la kumnyonyesha mtoto hadharani?

0 comments:

Chapisha Maoni